Somo la juma lililopita
tuliona japo kwa uchache sana madhara yaletwayo na mdudu msumbufu Mende,
nikukaribishe tena kwenye safu hili ya leo kuhusu hatua za maisha ya Mende na jinsi
ya kumzuia au kumwondoa ndani kwako bila kutumia sumu kali wala kemikali.
B:
HATUA ZA UKUAJI WA MENDE
Kama ilivyo kwa wadudu
wengi Mende huanzia hatua ya yai, na hupita hatua tatu hadi kifikia hatua ya
mwisho ya ukuaji mende mzima (adult).
Hatua hizo ni Yai;
Ni Muhimu ifahamike
kuwa kuna jamii nyingi sana za mende zaidi ya 4000 ambao huwa na tofauti
ndogondogo za maendeleo ya UKUAJI NA TOFAUTI ZINGINE ila kati ya aina hizi kuna
aina tatu wanaoishi majumbani mwa watu. Hapa naenda kuzungumzia zaidi wale mende ambao
wamekuwa ni tatizo kubwa kwa Watanzania na kwingineko duniani majumbani.
- Yai
Mayai ya mende yanakaa
ndani ya mfuko wa mayai wa rangi ya kahawia unaobeba wastani ya mayai 35
ujulikanao kitaalamu kama Ootheca (Fuko
la mayai). Ukubwa wa ootheca moja inakaridiwa kuwa mm 7 urefu na mm 2 upana
japo hutofautiana sana ukumbwa kati ya jamii moja ya mende na nyingine.
Kwa jamii nyingi za
Mende, dume huyarutumbisha viyai ndani ya jike na huendelea kujitengeneza ndani
ya ootheca. Jamii zingine za mende hubaki na mayai hayo na hukomaaa hadi
kuanguliwa ndani ya mwili na vifaranga huwa kama wanazaliwa; mfano kama vile Madagascar hissing cockroach.
Jike hutaga mayai
mfululizo anapofikia hatua ya mwisho ya ukuaji na kwa maisha yake yote ya
watani wa siku 100 kutegemeana na jamii ya mende. Mende mmoja anauwezo wa
kutaga mayai kwa makadirio kama 4oo hivi. Kwa aina ya mende waliozoeleka na
wanaopatikana kwa wingi nchini Tanzania hubeba mayai (ootheca) mwilini mwao
hadi linapobakiza siku mbili au siku chache kuanguliwa kisha hulitagia sehemu
salama na ngumu kufikika na binadamu. Mara nyingi mende jike mzima(adult)
huonekana akiwa na fuko la mayai mwilini mwake kila aendapo.
- Vifaranga (Nymph)
Vifaranga huanguliwa
vikiwa vidogo sana, rangi nyeupe, vilaini na hawana mabawa ambao hukua huku
wakibadili rangi hadi kufikia mende mzima. Vifaranga mara nyingi huanguliwa ndani ya siku
24 hadi 38 na idadi ya vifaranga vitakavyoanguliwa hutofautiana kutokana na
aina (Spicies) ya mende.
Vifaranga hupitia hatua
mbalimbali za kujibadili (molting) mpaka kufikia kuwa mende mzima. Vifaranga
(Nymph) na mwisho mende mzima na mara zote vifaranga (Nymph) ni mara tatu ya mende wazima yaani Vifaranga (nymph) 75% na
Wakubwa (adult) ni 25% ya mende wote waliopo kwenye makazi ya binadamu.
- Mende Mzima (Adult)
Japo kuna jamii za
mende ambazo hazina mabawa jamii nyingi wana mabawa, jamii hizi ambazo ni
wasumbufu sana ndani ya makazi ya watu nchini mwetu Tanzania na Africa
mashariki wana mabawa na huweza kuruka japo kwa umbali mfupi na hii huwa saidia
sana kusambaa kutoka kwa jirani mmoja hadi kwa mwingine. Mende hujifisha mchana
na usiku hula na kutembea.
Japokuwa mende ana uwezo wa kukaa bila kula
kwa muda wa miezi mitatu hawezi kuishi bila kunywa maji, Mende huishi kwa kula
mabaki ya vyakula, kunywa maji hula pia kwenye njia ya maji machafu na pia
chooni na wanaweza kuziba masinki kama wapo wengi sana kwenye nyumba.
Kwa asilimia kubwa
mende husambaa kupitia wasafiri hukaa kwenye mabegi, redio na viafaa vingine
vinavyosafirishwa na ukifika unako kwenda huhamia ndani ya nyumba.
Hotel nyingi zinapata mende kupitia wateja wao
wanaokuja kulala huleta mende bila kujijua
C) JINSI YA KUWAONDOA NA KUWAZUIA
WASIJE NYUMBANI BILA KUTUMIA WATAALAMU WALA
Kuna njia mbali mbali
za kupambana na mende nyumbani kwako bila kutumia wataalamu wa kupulizia sumu
au chemikali za kununua.
1.
Majani
ya Bei
(Laurus nobilis); mende
hawaupendi mmea huu na hivyo ukikatakata na kuweka sehemu sehemu za mende
kucheza na kula mende huondoka
2. Sumu ya mende ya kujitengenezea;
Chukua
kijiko kimoja cha chakula ya asidi ya boric changanya na vijiko viwili vya unga
wa mahindi na kijiko kimoja cha kokoa changanganya vizuri na nyunyiza sehemu
ambazo mende hupenda.
NB
mchanganyiko huu ni sumu hivyo weka mbali na watoto
3. Mtego wa mende;
Vaselini
uliotandazwa vyema kwenye kiboksi hunasa mende na hawataweza kutembea juu ya
vaselini. Ni vizuri kuweka chakula cha kuwavutia Mende ili waje kwenye mtego.
4. Mchanganyiko wa sabuni na Maji;
Changanya
sabuni ya maji na maji iwe nyepesi kiasi cha kuweza kupuliza kwa kutumia chupa
ya kupulizia. Kwa kutumia chupa ya kupulizia ama bomba ya kuogeshea mifugo
hakikisha unamdondokea mende, ikimdondokea tumboni ni vizuri zaidi. Matone
madogo mawili yakimpata mende tumbuni hufa baada ya muda mfupi
5. Amira (Baking Powder) and sugar;
Changanya
kwa uwiyano sawa sukari na amira (Baking Powder) kasha nyunyiza seheme mende
wanapenda kukaa sukari itawavutia kula na Amira itawauwa kwa kuwa fanya
wavimbiwe.
6. Sprei ya Nywele (Hair Spray);
Wapulizie
mende sprei ya nywele watakufa mara moja
7. Wanyime maji na chakula;
Kumbuka
mende wanahitaji maji kuliko wanavyohitaji chakula; hapa unashauriwa mabomba
yote yafungwe vyema yasiwe yanavuja maji, maji yakimwagika hakikisha
unayakausha kwa kudeki na kuacha nyumba yote kavu na sinki zote zifunikwe vyema
usiku na mchana pia kwa kutumia kizibo cha sinki; jokofu pia zisivuje.
Jitahidi
mabaki ya chakula yasibaki popote jikoni na chumba cha kulia chakula (dinning)
pia, vyakula vinavyobakizwa vivunikwe vyema kwenye bakuli mbalimbali na kuwekwa
kwenye jokofu au mahali pakuhifadhi chakula, vyombo vioshwe mara tu baada ya
kula. Kumbuka kipunje kidogo cha chakula kinawashibisha mende wengi hivyo
umakini kwenye hili unatakiwa.
8. Mchanganyiko wa Matango, pilipili
na Limao
Koroga mchanganyiko huu
kisha weka sehemu ambazo mende hupendelea kikaa/kuishi na mende watakimbia
ndani kwako hawatakaa.
Safisha
nyumba yako sana;
Anzia jikoni pawe
pasafi sana bila mrundikano wa vitu na vyombo visivyosafishwa. Vyakula
vilivyobaki vifunikwe vyema na kuwekwa kwenye jokofu.
9. Ficha chakula;
Chakula chochote
ambacho mende hula kitunzwe vyema sehemu ambapo mende hafiki kwenye jokofu pia
matumda huwapatia chakula na maji pia yatunzwe vyema
10. Safisha Sakafu;
Nasisitiza kuwa Mende
anahitaji maji ili kuishi jitahidi kuhakikisha hawapati maji kwa kusafisha na
kukausha sakafu; ondoa pia mabaki ya chakula, michirizi ya chakula na matone ya
chakula kwenye sakafu na ukutani au popote pale.
11. Ondoa chombo/debe la taka kila siku
Hii itawanyima chakula
mende ambao mara ngingi hujilisha ndani ya chombo cha taka pia nashauri chombo
taka cha nje kisikae sana karibu na nyumbu ili kuepusha mende wasiende
kujilisha huko usiku na kurudi ndani.
12. Maji ya Moto
Hii nimeshudia
sehemu/jamii nyingi za nchi yetu, maji huchemshwa na yanabaki yakiendelea
kuchemka na huchotwa kwa kutumia chombo na kuyarushia kwenye mikusanyiko wa
mende vifaranga na wakubwa haraka kabla ya kupoa. Hii ikifanyiki kila siku
mende huisha. Njia hii ni vizuri ikaendana na 9 hadi 12 kwa pamoja hizi
zitamaliza tatizo lamende bila kutumia sumu ama kemikali ambazo huitaji
mtaalamu ama garama kubwa.
D) KUZUIA MENDE WASIRUDI
- Ziba Nyufa
Nyufa za kuta za nyumba
pamoja na fenicha huwa makazi mazuri ya mende hivyo wanyime makazi hayo kwa
kuziba nyufa za fenicha na kuta za nyumba
Ziba nafasi kama vile
zile zilizopo kati ya kabati ya kujengea na ukuta kwa kutumia simenti au gundi
maalum ya mbao waweza kumshauri fundi afanye hivyo wakati wa kutengeneza kabati
na kama umepanga ama unaishi kwenye nyumba ya mwajiri basi jitahidi
kuhahakiosha hili linafanyika.
- Wazuie mende wasiingine ndani
Weka nyavu kwenye
madirisha na sehemu za kupitishia hewa kwenye nyumba pia milango iwekewe visuia
wadudu kwa chini na zibaki zimefungwa wakati wa usiku. Tundu lolote lisilo
(kioo, mbao, Ukuta nk) la lazima lizibwe.
- Epuka marundo ya mazao ya miti karibu na nyumba
Marundo ya mbao, kuni,
mabanzi, nk huwa ni kivutio cha mende hivyo yakiwa karibu na nyumba hupelekea
mende kuhamia ndani, hivyo nashauri zikae mbali na nyumba ya makazi.